MKUTANO WA INJILI ULIOENDESHWA NA PR MAPIMA
KANISA LA UKONGA SDA
TUWAPIME MANABII / MITUME WA SASA
KATIKA
MIZANI YA HAKI
____________________________________________________________________________________
§
UTANGULIZI
§
KWANINI KUWAPIMA WANAODAI NI MANABII?
§
MTU ANAKUWAJE NABII?
§
SIFA 5 ZA NABII, JE! WANAODAI NI MANABII TANZANIA
WANAZO SIFA HIZO?
§
JE! MIUJIZA NI KIPAUMBELE
AU KIINI CHA KAZI YA UTUMISHI YA NABII?
§
NA JE! MIUJIZA YA MANABII HAO KUANGUSHA WATU CHINI NI
YA KIBIBLIA?
§
ONYO JUU YA WATUMISHI WA UONGO KWA KIZAZI CHA NYAKATI
ZA MWISHO.
IMETAFITIWA NA
KUANDALIWA NA MCHUNGAJI- MHADHIR: DOMINIC MAPIMA
Utangulizi
Ninachukua fursa hii kwanza kukusalimu mpendwa msomaji
wa makala hii nyeti ya kuwachunguza Manabii na Mitume wanaoibuka katika
Ulimwengu lakini hususani katika nchi yetu ya Tanzania, Amani ya Bwana Yesu iwe juu yako!
Baada ya salaamu nipende kumshukuru sana Mungu Baba wa
mbinguni kwa kukuweka salama katika maisha yako hadi saa unapoisoma makala hii.
Mimi binafsi ninamshukuru Mungu pia kwanza kwa uzima,
lakini pili kwa kutimiza shauku yangu ya kiutafiti na uandishi wa makala hii
ili kufungua macho watu wa Mungu wanaobaki kuchanganyikiwa au kutekwa na hali
hii ya sintofahamu ya kuibuka kwa wimbi kubwa la watu wanaodai kuwa ni
watumishi, mitume na manabii na kufanya maajabu mbalimbali na miujiza huku
wakidai haki ya kuaminiwa na kukubalika kama sehemu ya mitume na manabii wa kweli
wa Mungu wa kibiblia.
Kabla ya kuandika makala hii nilisumbuka kwa muda
mrefu ndani ya moyo wangu kuona hali hii ikishika kasi katika nchi yetu ya
Tanzania kwa kiwango cha juu na zaidi kukutana na watu mbalimbali walioumizwa
na vuguvugu hili la kuibuka kwa watu hao wanaodai kuwa ni watumishi tena katika
daraja hilo la mitume au manabii.
Msukumo wa kuandika makala hii kutokana na shuhuda za
kitapeli ‘
ü Nikiwa katika
mahubiri mnamo mwezi wa 9/2011 katika eneo la kidatu, dada mmoja alikuja kwenye
mkutano akiwa na bahasha yenye pesa’ baada ya kuhojiana na wahudumu wa kwaya
alijieleza kuwa ameleta bahasha hiyo baada ya kuhudhuria mkutano Fulani ambapo mhubiri
alijitambulisha kama mtume na Nabii’_mhubiri huyo aliwataka wenyeshida
mbalimbali waende wakaombewe ambapo dada huyo pia alijitoa kwenda kuombewa’
baada ya maombi hayo, mtumishi (mtume) huyo alitangaza kuwa wote walioombewa
wanapaswa kupeleka sadaka ya Tsh 3000/= kama shukrani ili Mungu aridhie maombi
yao Na kama wasingefanya hivyo wangeweza kufa,hivyo dada huyo kwa hali duni
sana ya maisha aliyokuwa nayo alichelewesha kupelekwa fedha hiyo’ na kwakuwa
mkutano ulishakuwa umefungwa basi aliamua kuleta fedha hiyo mkutanoni kwetu kwa
kudhani kuwa sisi tuko pamoja na mtumishi huyo. Ili kuepuka hukumu hiyo.
Mpendwa msomaji wangu, tendo la kukutana na tukio hili
lilizidi kuamsha msukumo niliokuwanao moyoni mwangu wa kuandika makala hii
maalumu ya Kibiblia ili kusaidia maelefu ya watu waliofungwa kihisia na kiimani
hivyo kuzama katika kuwaamini watumishi hao wa uongo.
Msukumo wa
kuandika makala hii kutokana na kuhushwa hadhi cheo cha Unabii, Utume‘
Msukumo wa
kuandika makala hii kutokana na Wimbi la maombezi na Miujiza ya ajabu‘
TUCHUNGUZE IMANI
Pr Dominic
Mapima.
Somo la ‘8’ Mahubiri ya
hadhara – Ukonga SDA.
NEEMA NA SHERIA KATIKA JUKWAA LA UTAKASO
UTANGULIZI
PAMOJA NA KUJIFUNZA KWA
KINA JUU YA KIOO CHA MSAFIRI WA IMANI YAANI SHERIA AU AMRI KUMI ZA MUNGU NA
UMUHIMU WAKE KWA WAFUASI WA IMANI, BADO LIKO HITAJI JINGINE LA KUFANYA MAPITIO
YA MADA HII ILI KUWEKA BAYANA UKWELI JUU YA DHANA MBALIMBALI ZISIZO SAHIHI
ZINAZOIBUKA JUU YA SHERIA ZA MUNGU KWA KILE KINACHODAIWA KUWA SHERIA HIZO ZA
MUNGU ZILIKOMA KUFUATIA TENDO LA KIFO CHA YESU MSALABANI, KIFO AMBACHO
KILIFUNUA KITU KINACHOITWA ‘NEEMA’ (MSAMAHA WA BURE).NA HIVYO KUDAIWA KWAMBA
NEEMA HIYO INAONDOA AU KUKOMESHA SHERIA’ (AMRI KUMI).
KATIKA KUWEKA MSISITIZO WA MADAI HAYO, WALIMU NA
WAHUBIRI HAO WALIOIBUA FARSAFA HIYO WAMEKUWA WAKITUMIA MAFUNGU KADHAA YA
MAANDIKO YA BIBLIA KWA KILE KINACHODHANIWA KUWA MAANDIKO HAYO YANAUNGA MKONO
FARSAFA HIYO YENYE UTATA
Efeso 2;8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwanjia ya imani, ambayo
hiyo haikutokana na nafsi
zenu,ni kipawa cha Mungu. (9) wala si kwa
matendo, mtu awaye yote asije
akajisifu.
Galatia 3:11Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za
Mungu katika sheria, kwasababu mwenye haki ataishi kwa imani.
Hayo ni baadhi ya mafungu ya Biblia yanayotumiwa
kukaza hoja hiyo juu ya kile kinachodaiwa kuwa mafungu hayo yanatoa madai
ya kutokuwepo kwa umuhimu tena wa sheria za Mungu kutokana na mafunuo ya neema ya Kristo kwa kifo cha masalaba
na hivyo wenye haki wa Mungu wataishi kwa imani na hakuna haja tena ya sheria
au amri za Mungu katika maisha ya muumini.
HIVYO BASI’ KUPITIA SOMO HILI TUTAANGALIA KWA UMAKINI
ILI KUPATA UELEWA WA MSINGI JUU YA MAHUSIANO YA NEEMA NA SHERIA KATIKA JUKWAA LA
UTAKASO, LAKINI PIA KUONA KAMA MADAI HAYO NI YAKWELI AU NI TAFSIRI TU
INAYOTOLEWA KAMA MATOKEO YA KUTOYASOMA MAANDIKO KWA UMAKINI.
KOSA LA
UMAKINI KATIKA USOMAJI WA BIBLIA
Kile kinachoonekana kuwa ni tatizo la waalimu wengi
wanaeneza farsafa hii isiyo sahihi, ni uelewa husiyo wa kina juu ya mfumo mzima
wa mafunuo ya “sheria” katika maandiko ya Biblia.
Ni kosa kubwa sana katika taaluma ya usomaji wa Biblia
kutojua muundo wa mafunuo ya sheria hivyo kutoweka tofauti unapojadili au
kusema lolote juu ya mafunuo hayo ya sheria,
na pengine niseme kuwa hata changamoto hii ya madai ya kukomeshwa sheria (amri kumi) imezaliwa kutokana na makosa
hayo ya wale wanaofundisha kutokuwa na kina cha uelewa juu ya mifumo ya sheria
katika Bilblia na hivyo kuelewa kazi za sheria katika aina zake na uhusiano
wake na neema ya Kristo kwa kifo cha
masalaba.
Walimu wengi leo wanasoma Bibli kwa kubahatisha/
tumekuwa kama vipofu.
Mfano;
Eg; kulikuwa na vipofu wawili ambao walitamani kufahamu
umbile la tembo,bahati njema Serikali yao iliandaa fursa maalumu kwa walemavu
kwenda kufanya utalii wa kufahamu wanyama hao,wakiwa katika banda maalumu
alipohifadhiwa tembo aliyetulizwa kwa madawa maalumu, vipofu hawa waliingizwa
kwa zamu ili kumgusa tembo huyo, ili kufahamu umbile lake’ kipofu wa kwanza-alimgusa
kwa hofu kubwa kwenye mkonga akishusha na kupandisha mkono’ na ghafla aliruka
kwa shangwe huku akidai kuwa amegundua kwamba tembo anafanana na nyoka!!!’/ kipofu
wapili naye –alishika eneo la sikio la tembo na kupitisha kiganja mithili
ya mtu anayesuuza chombo ndipo naye ghafla alionekana kurukaruka huku akidai
kuwa tembo anafanana na sahani ya kulia ugali!!!
Kimsingi vipofu hawa wote walipata nafasi ya
kumchunguza tembo, lakini kile kinachoonekana kuwa ni kosa kwao ni aina ya
uchunguzi na viwango vya uchunguzi wao huo viliwaletea majibu yasiyoendana na
ukweli halisi juu ya umbile hasa la mnyama huyo’ tembo. Kosa hili ndilo
linalotendwa katika ulimwengu wa kidini leo na hivyo kupelekea kuibuka kwa
farsafa mbalimbali zisizo za haki hivyo kuwachanganya wafuasi waaminifu wa dini.’
KUWEKA TOFAUTI YA SHERIA KATIKA BIBLIA.
Kanuni ya kwanza muhimu katika ufumbuzi wa changamoto
hii ni kuchunguza mfumo wa sheria katika Biblia, inaweza kuwa swala rahisi kuelewa
mafungu mbalimbali ya Biblia yanayozungumzia kukoma kwa sheria nk, ikiwa tu
tutakuwa na uelewa sahihi juu ya muundo wa mafunuo ya sheria katika Biblia.
Mungu alipofunua sheria zake aliweka tofauti, hivyo
pamoja na kuwepo kwa makundi mengi ya sheria tunaweza kufanya migawanyo ya
ufupi ya sheria kama ifuatavyo:-
Moral Laws – Sheria adilifu’
Social Laws – Sheria za kijamii’
Ceremonial Laws – Sheria za sherehe za makutaniko na kafara’
Huo ni mgawanyo mdogo wa mafunuo ya sheria katika
maandiko ya Biblia, hivyo utagundua kwamba kwa kadri ya Biblia unapozungumzia
sheria unaongelea uwanja mpana sana wa kiuchambuzi.
Namna Biblia inavyoweka
tofauti ya sheria
Biblia inagawanya sheria hizi katika makundi makuu
mawili ya msingi.
Moral Laws – Sheria adilifu,
“amri kumi za Mungu” – hili ni kundi muhimu sana la la sheria (amri) za
Mungu, Biblia inaweka tofauti ya sheria hizi na zile nyingine za kijamii yaani Social Laws na Ceremonial Laws, na kwajumla kundi hili la pili hutajwa kama “sheria za Musa au Sheria za maagizo”, hivyo
pia maandiko ya Biblia yameweka kanuni bora ya jinsi ya kuweka tofauti ya
sheria hizi kama ifuatavyo:-
1. Tofauti ya kwanza.
§ Amri kumi ‘Moral Laws’ – Ziliandikwa na Mungu mwenyewe Kutoka 31:18.
§ Sheria za Musa/Maagizo’- Ziliandikwa na Musa 2nyakati 35:12.
2. Tofauti ya pili.
§ Amri kumi’ Moral Laws’- Zilihifadhiwa katika sanduku la agano. Kumb 10:5
§ Sheria za Musa/Maagizo- Ziliwekwa kando ya sanduku.
Kumb 31:24 -26
Kwa msingi huu wa mgawanyo wa Sheria ,unaweza kugundua
kuwa kabla mtu hajajenga hoja yeyote juu ya sheria lazima ajue aina ya sheria
anazozikusudia.
Na kutokana na kutozingatia hilo baadhi ya viongozi na
wahubiri wa dini wamesikika wakitoa tafsiri na maelezo ya jumla yanayogusa
mustakabali wa sheria hizi pasina kuweka tofauti yeyote tendo liliozua tafsiri
batili kuwa kifo cha Yesu kililenga kukomesha aina zote hizo za sheria, na
hivyo kwasasa sheria za Mungu hazina
kazi tena katika maisha ya waumini kwa kuwa tunaishi kipindi cha neema.
JE’ NI AINA
GANI YA SHERIA INAYOKOMESHWA NA NEEMA?
Kwa kujifunza mgawanyo huo wa sheria katika Biblia,
ndipo unaweza kujiuliza swala hilo la busara kuwa je’ mauti ya Yesu au Neema ya msalaba
inakomesha aina gani ya sheria? ni zile adilifu (amri kumi – moral laws)
au ni zile za Maagizo? (Sheria za Musa/ceremonial laws – social laws)?.
Neema haikukomesha amri
kumi ( Moral Laws) bali amri (sheria) za maagizo.
Tunapozungumzia neema maana yake tunazungumzia mauti
ya Yesu msalabani iliyoleta msamaha wa bure husiyotokana na kustahili
kwetu,msingi au kusudi la mauti ya Yesu ilikuwa ni kutimiza madai ya torati juu
ya utakaso wa dhambi na ukombozi wa nafsi..
Ebrania 9:22 Na katika Torati vitu vyote husafishwa kwa damu na pasipo
Kumwaga damu hakuna ondoleo.
Madai hayo ya torati hapo awali yalitimizwa kwa njia
ya kuchinja wanyama maalumu kama tendo la kafara au fidia ya uovu na makosa ya
mwanadamu kwa Mungu ambapo maelekezo hayo ya uchinjaji wa wanyama kama ishara au kielelezo cha neema iliyokusudiwa kuja ndiyo
yaliyotambuliwa kama sheria za makafara’
Ceremonial Laws’, kwa msingi huo Yesu alipokufa msalabani alichukua nafasi
ya wanyama hao nay eye kuwa ndiye kafara halisi ya dhambi zetu, na hivyo kwa
hali hiyo ile sheria ya uchinjaji wa wanyama inakoma.
Kwa muktaza huo inakuwa ni sahihi kusema kuwa neema ya
Yesu imekomesha sheria hiyo kwamaana sasa watu hawana haja tena ya kuchinja
wanyama kama tendo ya kafara ya dhambi kadri ilivyoamriwa katika sheria ile ya
makafara. Rejea:- lawi 22:19-21/ lawi 23;26.
Lakini kile kinachoonekana ni kuchanganya mawazo ya
Kibiblia, ni pale baadhi ya wahubiri wanaposikika wakihubiri kwa ujasiri kuwa
mauti hiyo ya Yesu ililenga kukomesha aina zote za sheria, na hivyo sasa
tunaishi chini ya neema hivyo hakuna haja tena ya amri , sheria za Mungu
wakimaanisha kuwa hata amri zile kumi (adilifu zilizoandikwa na Mungu mwenyewe)
zimekoma, na hakuna haja ya kuwekea maanani amri hizo’ fundisho hilo ni la
hatari sana.
AMRI KUMI NI
ZA MILELE, ZINAFANYAKAZI NA NEEMA.
Mbali na sheria hizo nyingine za maagizo
zinazokomeshwa na mauti ya Yesu msalabani, amri kumi za Mungu zilizoandikwa
kwenye mbao za mawe zinadumu milele, kimsingi amri zile kumi ndiyo tabia halisi
ya Mungu anayohitaji sisi wanadamu tuiakisi ili tudumu kuitwa wana na binti
zake.
Mambo yanoyothibitisha kuwa amri hizo ni za kudumu.
-
Ziliandikwa kwa kidole cha Mungu mwenyewe “Mhubiri
3:14.
-
Ziliandikwa kwenye mbao za mawe; ni ishara ya kudumu.
“Kumb 9:9-11
-
Biblia inazitaja ni za milele “Zaburi
Sababu ya msingi ya kudumu kwa amri kumi:-
-
Ndiyo kauli mbiu ya Mungu juu ya vile mwanadamu
anavyopaswa kuenenda na hivyo kuakisi tabia yake. “Zaburi
40:8 kuyafanya
mapenzi yako.... ndiyo furaha yangu,.... sheria yako imo moyoni mwangu
-
Ndicho kipimo cha haki na ubatili, kuelewa imani
sahihi, watumishi wa kweli na wauongo wanapimwa kupitia mwenendo wao na utii wa
amri hizi.
Isaya
8:20 Na waende kwa sheria na
ushuhuda kama hawaendi sawasawa.....
-
Ndiyo msingi wa kazi ya kanisa duniani, kwakuwa kazi
ya kanisa ni kutangaza mapenzi ya Mungu ambayo kimsingi yanafunuliwa katika
amri zake, hivyo kanisa lipo ili kutangaza mapenzi ya Mungu(amri /sheria zake)
Yohana
14:15 mkinipenda
mtazishika amri zangu.
-
Amri za Mungu zinadumu pia kwasababu bado huduma ya
upatanisho wa dhambi inaendelea katika hekalu la mbinguni na amri za Mungu ni
shahidi wa matendo kama ilivyokuwa katika hekalu la dunia.
Ufunuo
11:19 Hekalu la Mungu lililoko
mbinguni likafunguliwa..na sanduku la agano lake likaonekana mbinguni....
Kwa uchambuzi huo wa maandiko unaweza kugundua ndugu
msomaji kuwa amri kumi za Mungu ndiyo uti wa mgongo wa kusudi zima za Mungu
kushughulika na wanadamu, na jambo lenye uzito zaidi ni kuwa neema ya Yesu
msalabani ili ifanyekazi lazima kuwepo na sheria/ amri za Mungu.
Kazi ya Neema na Sheria/
je Neema inaondoa sheria?.
Neema ni nini? – Ni msamaha
wa bure unaotolewa na Mungu kwa huruma
zake
kwa mwanadamu mdhambi pamoja na kutostahili
kwake.
Sheria ni nini? -
Ni mafunuo ya maelekezo au
maagizo ya tabia na usafi wa
Kiroho ns kimwenendo
anaopaswa kuwa nao mwanadamu ili
kuunganishwa
kitabia na Mungu.
Uhusiano wa Neema na Sheria’
Kazi ya Neema:
Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
(11)nayo yatufundisha kukataa
ubaya na tamaa za kidunia; tupate
kuishi kwa kiasi, na haki, na
utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa.
Andiko hili ndilo linalofunua kazi ya Neema’ na kama
umefatilia vizuri fungu hilo utagundua kuwa kwajumla kazi ya Neema ni kutoa
uwezo wa ushindi kwa mwanadamu dhidi ya matendo ya dhambi.
Kwakuwa kazi ya Neema ni kumwezesha mwanadamu
kuishinda dhambi basi utagundua kuwa ili Neema ifikie kusudi hilo lazima
isaidiane na sheria kutokana na kazi ya sheria inayoelezwa kupitia kitabu cha
Warumi, hebu tusome:-
Warumi 7:7 Tusemeje basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua
dhambi ila kwa sheria; kwakuwa singalijua
kutamani, kama Torati
isingalisema, usitamani.
Hivyo dhambi hujulikana kwa njia ya sheria, na
tutakubaliana ndugu msomaji kuwa haiwezekani kupambana au kuishinda dhambi
ikiwa hujui kuwa hiyo ni dhambi’;“Hata
wachezaji wa mpira hawaendi katika shindano pasipo kujua uwezo na mbinu za timu
pinzani’ huweza hata kutuma watu kupeleleza wenzao’.
Kwahiyo kimsingi, Neema na Sheria hufanya kazi pamoja,
yaani Sheria hufunua dhambi na Neema hutoa uwezo kwa mdhambi kuishinda.
Kwamaana hiyo’ si jambo sahihi kutafsiri kuwa Neema
imekuja kuondoa sheria za Mungu ( Amri kumi)., na kwadri ambavyo Neema na
sheria hufanyakazi kwa pamoja, kusema kuwa Neema imeondoa sheria kunamuingiza
mtu anayedai hivyo kwenye kosa pana la kufuta kabisa uwepo wa kanisa,
kwasababu:-
“Bila sheria HAKUNA DHAMBI/ kama
hakuna dhambi basi HAKUNA HAJA ya NEEMA/ na kama hakuna neema basi HAKUNA
MSALABA/ kama hakuna msalaba basi hakuna WOKOVU/ kama hakuna wokovu basi HAKUNA
KRISTO MWOKOZI/ kama hakuna Kristo basi hakuna UKRISTO/ kama hakuna ukristo
basi HAKUNA KANISA”
Mfano
Utendaji wa
Sheria na Neema.
Eg; Neema na
Sheria ni sawa na Trafic na Garage/ ikiwa umepata ajali kwa gari yako kugongwa
na gari nyingine, huwa anaitwa Trafiki, kazi ya Trafiki ni kuonyesha kosa ni la
nani kwa mujibu wa sheria, hivyo Trafiki ni Sheria’na baada ya funua mkosaji si
jukumu lake kuombwa kutibu madhara ya ajali kwa kunyoosha gar ink, jukumu hilo
hufanywa na gereji’ hivyo gereji ndiyo neema. Hivyo huwezi kusema kwasababu
tuna geriji za kunyoosha magari basi hakuna haja ya sheria za barabarani.
Mfano
Sheria
zinakuonyesha kosa nawe unatafuta Neema.
Eg; kibaka mmoja alipora mtu simu,
watu walimkimbiza wakiwa na silaha kali, hatimaye wakafika mahali ambapo
kulikuwa na njia 2’ moja ni ndefu sana ambayo kama angepita hiyo wangeweza
kumpata, lakini njia ya pili ilikuwa ikielekea kituo cha polisi, kwa kadri ya
hatari hiyo alitambua kuwa kwa ukosaji huo ni bora ajisalimishe polisi ambapo
labda angepata rehema na kuepuka mauti’...sheria inakufanya utambue kosa, na
kosa hilo litakuongoza kuitafuta neema kwa kuwa utajiona kuwa ni mhitaji.
Hatari kwa wanaokataa sheria’
Kile kinachoonekana kuwa ni hatari kwa wale wanaopinga
mafunuo ya sheria ni hisia za kujiona wenye haki.
Kumbuka neema inahitaji mtu anayejiona kuwa ni mdhambi
anapojipima mbele za MUNGU ili apate rehema, visa na mafungu yafuatayo vinaweka
wazi:.
1yohana 1:8-10 tukisema kwamba hatuna
dhambi twajidanganya
Mathayo
Sadukayo na farisayo walikwenda kuomba, Farisayo
alijihesabia haki,
lakini Sadukayo alisema yeye ni mwenye
dhambi..huyu ndiye
aliyekubaliwa toba yake....
MAFUNGU YANAYONESHA KUDUMU KWA AMRI ZA MUNGU KATIKA
AGANO JIPYA
Katika kipindi cha injili bado Mungu aliendelea
kusisitiza juu ya ya umuhimu wa kutunza amri na sheria zake, kupitia kwa kinywa
cha Yesu mwenyewe na mitume wake’
Unaweza kusoma mafungu yafuatayo kuona jambo hili la
msingi’
Mathayo
19:17 ..ukitaka kuingia ufalme wa Mungu shika amri..
Luka 1:5 ....Zakaria na Elizabeti walishika amri zote za Bwana..
Rumi 8:3 ...maagizo ya Torati yatimizwe ndani yenu...
1wakoritho
9:20 ... Ni mwenye sheria mbele za Kristo..
Watu wa kihistoria
waliopenda amri za Mungu”
Msafiri mvumbuzi Sir HENRY
MORTON STANLEY – alimsomea Chief wa
Afrika amri kumi/ naye aliomba watu wake wafundishwe amri hizo, alisema endapo
watu wake wakijua amri hizo atakuwa mfalme pekee mwenye taifa lenye watu wenye
upendo wa kweli’.
Mwanafarsafa Emmanuel Kant, aliwahi kusema; hakuna sehemu tukufu
katika maandiko ya Kiebrania kama amri kumi.
Maswali ya kujadili juu ya wale wanaopinga Sheria za
Mungu’
-
Kama amri hizo hazina haja tena sasa, kwanini
wanawaongoza watu wao kutubu, nini kimefanya wajue kuwa wanapaswa kutubu
tofauti na sheria?
-
Kwanini wanakemea dhambi kama vile, wizi, uzinzi,uongo
nk je ni nini kilichowajulisha kuwa hizo ni dhambi? Na kama amri hizo
zilishaondolewa msalabani kwanini wanaendelea kuzihubiri na huku kwa upande
mwingine wanazikanusha? Au ni nini hasa wanachojaribu kukwepa katika amri ,hdi
kuonyesha kutokuwa na msimamo tulivu wa kifikra juu ya amri za Mungu?
Nyongeza ya
sheria za maagizo zilizoondolewa na mauti ya Yesu.
Ninaamini mpendwa msomaji wangu tuko pamoja katia
mfululizo huu wa uchambuzi juu ya Sheria na Neema, ninapoelekea ukingoni kwa
uchambuzi huu nimeona vema pia nikupatie mwangaza kidogo juu ya aina ile
nyingine ya Sheria za Maagizo au Makafara zilizokomeshwa’
Pitia kwa utulivu sheria hizo katika maandiko mawili
hapo chini, ili kuona sheria hizo ambazo Yesu alizisitisha mbali na zile amri
kumi adilifu za milele.
Lawi 15:19-28
Lawi 21:1-22
-
Sheria za kafara za wanyama
-
Tohara
-
Unajisi wa damu ya hedhi na shahawa.
-
Unajisi wa wakoma.
-
Unajisi wa kushika maiti.
Kadri ya Bblia sheria hizo na nyinginezo kadhaa zilikuwa
ni sheria za mpito na zilipaswa kukoma baada ya ujio wa Masihi /Yesu alifanya
matukio kadhaa kama ishara ya kukomesha sheria hizo”...
-
Aligusa wakoma – Mathayo 9;18-25
-
Aliguswa na mwanamke waliyetokwa damu- Marko
5:25-34
-
Aligusa na kufufua maiti wakati wa huduma yake.
Amri kumi za Mungu zinadumu milele zote / Ufunuo 14:12
TUCHUNGUZE IMANI
Pr Dominic
Mapima.
Somo la ‘9’ Mahubiri ya
hadhara – Ukonga SDA.
MUNGU MMOJA ’ SIKU MOJA YA IBADA
TUMEKWISHA KUONA KUPITIA
SOMO LA “KIOO CHA MSAFIRI” JUU YA MAFUNUO YA SHERIA“AMRI KUMI ZA MUNGU”.KWA
NAMNA YA UPANA TUMEONA UMHUHIMU NA KAZI YA SHERIA KWA WAFUASI WA DINI KUWA
SHERIA NDICHO KIOO CHA KUTUSAIDIA KUTAMBUA HALI YETU YA KIMAHUSIANO NA MUNGU,
KUWAPIMA WOTE WATAKAOIBUKA NA KUDAI KUWA NI WATUMISHI PAMOJA NA KUTUSAIDIA
KUTAMBUA IMANI YA KWELI NA YA UONGO.
LAKINI IKIWA UTAKUMBUKA KATIKA UCHAMBUZI WA SHERIA
“AMRI” HIZO KUMI ZA MUNGU TULIONA MOJAWAPO YA AMRI IKIGUSA JUU YA SWALA LA
IBADA; fatilia rejea ya amri hiyo ya nne’
Kutoka
20:8-11 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. (9)siku sita
fanyakazi, utende
mambo yako yote, (10) lakini siku ya Saba ni
Sabato ya BWANA,
Mungu wako, siku
hiyo usifanye kazi yeyote,wewe, wala mwana
wako, wala mjakazi
wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala
mgeni aliyendani ya malango yako.(11)Maana,
kwa siku sita
BWANA alifanya mbingu,
na nchi, na bahari, na vyote
vilivyomo,akastarehe
siku ya saba; kwahiyo BWANA akaibarikia
siku ya Sabato akaitakasa.
Kulingana na makusudi hayo ya sheria niliyoyainisha
kwa kifupi hapo juu kama ilivyo katika somo la kioo cha masafiri, tutakubaliana
kuwa ni jambo muhimu sana kuichunguza kwa kina amri hii ya ibada ili pia
itusaidie kujipima na hatimaye kuona kama mwenendo wetu katika mifumo ya ibada
inakubaliana na maelekezo ya mwabudiwa au vinginevyo!Hivyo nitoe wito kwako mpendwa msomaji wangu kuwa makini katika uchambuzi
wa mada ili kupanua maarifa.
KWANINI
MUNGU ALIWEKA MAELEKEZO JUU YA IBADA?
Ni jambo la busara kwanza kabla ya kusonga mbele na
uchambuzi wa mada hii tukajiuliza swali hili muhimu kwamba kuna sababu zipi za
msingi zilizofanya Mungu aweke malekezo ya ibada katika amri zake!, pasipo kuchukua muda ningependa
kueleza moja kwa moja sababu mbili muhimu kama ifuatavyo:-
Sababu ya 1,
Yeye ndiye mwabudiwa hivyo ndiye hasa
anayepaswa kumpa maelekezo mwanadamu vile anavyoweza kufanya katika swala zima
la kumwabudu.
Isaya
45:22-23 Niangalieni mimi, mkaokolewe ,enyi ncha zote za
dunia; maana
mimi ni Mungu; hapana
mwingine.
Katika swala la ibada msikilize Mungu tu usimsikilize
mwanadamu.
Mfano:
binadamu hatokuokoa.
Eg; wakati wa
vita ya Uganda Mhindi alisikia mlio wa bunduki na kuanza kukimbia akiwa
amesahau mtoto kitandani, na alipokumbuka na kurudi kumwokoa ndipo alipojikuta
anaondoka na paka aliyeenda kujificha kwenye kitanda hichohicho kwa kujifunika
sambamba na mtoto.
Sababu ya 2,
Shetani naye anadai kuabudiwa na
wanadamu, na daima anapinga Mungu wa kweli kuabudiwa, hivyo maelekezo juu ya
namna ya kumwabudu Mungu wa kweli ni kanuni pekee ya kumwezesha mwanadamu kuwa
na hakika kuwa ibada yake hiyo ni ya kumwelekea Mungu wa mbinguni.
Mathayo 4:9-10 akamwambia, haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. (10)
Ndipo Yesu akamwambia
, Nenda zako shetani, kwamaana
imeandikwa, msujudie
Bwana Mungu wako, umwabudu yeye
peke yake.
Matakwa ya shetani pia ni kuabudiwa, hivyo ni mpinzani wa ibada kwa Mungu.
KEMEO LA
YESU JUU YA IBADA ZISIZOFATA MAELEKEZO YA NENO.
Katika kuweka mkazo wa kuchunguza amri hii ya maelekezo
ya ibada, ni vyema pia kuangalia jinsi Yesu mwenyewe alivyoonyesha hatari ya
kupuuzia maelekezo ya Mungu juu ya ibada’.
Mathayo 7:21Si kila mtu aniambiaye , Bwana Bwana ,
atakayeingia katika
ufalme wa mbinguni;
bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu
aliye mbinguni.
Marko 7:7-13 Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyomaagizo ya
wanadamu, (12) Ninyi
mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika
mapokeo ya wanadamu.
Ninaamini msomaji wangu umeona jinsi Bwana Yesu
mwenyewe alivyoweka bayana na kukaza umuhimu juu ya kujenga msingi wa ibada na
mifumo yetu ya kidini katika maelekezo halali ya Mungu mwenyewe na si badala
yeke kufata au kutii sauti za wanadamu mahali pa sauti na maelekezo ya Mungu
mwanyewe.’
MAELEZO YA
YESU JUU YA KANUNI YA IBADA YA KWELI.
Bwana Yesu pamoja
na mambo mengine katika maelezo yake aliweka wazi kanuni ya msingi ya ibada ya
kweli, swala hili pia linatilia mkazo hoja yetu ya msingi tuliyokwisha ijadili
juu ya sababu ya Mungu kuweka maelekezo ya ibada, kupitia maandiko yafuatayo
tunaweza kugundua kipimo halisi cha ibada ya kweli na hivyo kutupa ujasiri
mkubwa wa kuanza kuchunguza kwa makini amri ile ya Mungu juu ya ibada’;
Yohana
4:24
Mungu ni roho nao wamwabudio yeye imewapasa kumwabudu
katika roho na kweli.
Andiko hilo maarufu
la Biblia ndilo linalofunua kanuni ya ibada ya kweli, katika maelezo hayo Bwana
Yesu anataja mambo makuu mawili ya msingi juu ya kanuni ya ibada ya kweli, nayo
ni;
-
Kuabudu
“katika roho”
-
Na “Kweli”
Kanuni
hizo mbili ndizo msingi wa ibada ya kweli, kwa maana nyingine endapo muabudu
atapungukiwa na mojawapo kati ya hizo basi anajiingiza mwenyewe katika karipio
la Yesu juu ya wale wanaoabudu kwa kufata mapokeo ya wanadamu badala ya sauti
ya Mungu.
Kwanini
kuabudu katika Roho na Kweli?
“Kuabudu
katika roho’ _
Kuwa na ibada halisi ya kumaanisha , inayoanzia
Katika chimbuko halisi la utu wa ndani.
“Na ‘Kweli” Ni Ibada iliyojengwa katika mfumo au taratibu
halali zilizoamriwa
na Neno la Mungu / imeelekezwa na kumriwa na
Mungu.
Yohana
17:17
Uwatakae kwa ile kweli, Neno lako ndiyo kweli.
JE’
NI IPI BASI IBADA ILIYOAMRIWA NA NENO LA MUNGU?
MUNGU
MMOJA ’ SIKU MOJA YA IBADA
Ni jambo
linalochanganya hisia za waumini wengi wa kidini kwa karne nyingi sasa juu ya
kuelewa siku halisi moja ya ibada iliyoamriwa na Mungu, uchunguzi unaonyesha
kuwa asilimia kubwa ya waumini wanaabudu lakini baila kutilia maanani swala
zima la kuchunguza endapo mfumo au siku ya ibada wanayokutanika kusali ndiyo
iliyoamriwa na Mungu au vinginevyo!.
Furaha ya waumini
wanapokuwa katika ibada zao, kucheza na kuombewa mahitaji yao ndivyo vimekuwa
vigezo vya kuhisi kukubalika kwa ibada yao na hivyo kutokuwa na muda kabisa wa
kuona kama wamejengwa katika roho na kweli kadri ya maelekezo ya Yesu juu ya
kanuni ya ibada halisi’.
Ikumbukwe kuwa Bwana
Yesu alilaumu na kukemea hali hiyo, kama ishara ya kutokukubaliana nayo:-
Marko 7:7-13 Nao waniabudu bure, wakifundisha
mafundisho yaliyomaagizo
ya wanadamu, (12) Ninyi
mwaiacha amri ya Mungu, na
kuyashika mapokeo ya
wanadamu.
Swali’: ni siku gani
hiyo ya ibada iliyojegwa katika msingi wa amri ya Mungu?
Chimbuko
la siku ya Ibada ya kweli’
Siku ya ibada ya
kweli katika Biblia inatajwa kuwa na chimbuko la aina ya pekee linaloonyesha
umaalumu wake usiyoweza kugeuzwa na yeyote.
Huenda litakuwa ni
jambo la kukushangaza kusikia kuwa siku hiyo ya ibada iliumbwa”, hii ni
kumaanisha kuwa tangu Mungu alipoweka misingi ya dunia pia aliweka mfumo wa
ibada, alipokuwa akiumba alikumbuka kuwatengenezea watu wake mazingira na
utaratibu maalumu wa kuabudu kwa kutenga siku moja aliyoiweka maalumu katika
uumbaji kwa kusudi hilo la ibada.
Hebu ona:-
Mwanzo
2:1-3
Basi mbingu na chi zikamalizika, na jeshi lake lote.(2)Na siku ya
saba Mungu alimaliza
kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku
ya saba,akaacha kufanya kazi yake yote
aliyoiumba na
kuifanya.(3)Mungu akaibarikia
siku ya saba, akaitakasa
kwasababu katika siku
hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya
kazi yake yote aliyoiumba
na kuifanya.
Naamini kupitia
andiko hilo umeweza kuona kile nilichotangulia kusema hapo awali, kwa hali
halisi Mungu alipokuwa anaumba alishabuni utaratibu mzima wa mwenendo wa dunia
katika mfumo wa siku, ambapo aliumba juma moja lenye siku saba’, huwa tunaimba
hata shuleni:-
“How many
days in the week!!!! Kiitikio’ Seven days x 2
“Kuna siku ngapi katika juma!!! Kiitikio’ Siku saba x2
Hivyo katika mfumo
huo wa juma moja la siku saba, Mungu tangu katika uumbaji wake alishatenga siku
moja ambayo pamoja na mambo mengine Biblia inasema aliibariki na kuitakasa (neno takasa katika chimbuko lake la lugha asilia
lilikusudia “Kutenga kwaajili ya mambo matakatifu”).
Katika kuthibitisha
uhalali wa mfumo huo aliouweka, Mungu mwenyewe alionyesha kielelezo kwa tendo
la yeye mwenyewe kustarehe katika siku hiyo,rejea maelezo ya andiko la kitabu
cha Mwanzo 2:2….akastarehe siku ya saba;
akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
Mgawanyo
wa siku katika mfumo wa uumbaji.
Kuonyesha kuwa
Mungu aliweka makusudi yake katika mfumo wa uumbaji hususani juu ya swala hili
la ibada ya siku hiyo ya saba(sabato), maandiko yanaonyesha kile
alichokiweka Mungu katika anga ili
kuzalisha mfumo mzima wa majira katika mzunguko wa dunia.
Mwanzo
1:14
Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge
kati ya mchana na usiku;
nayo ndiyo iwe dalili ya majira na siku na
miaka.
Biblia inataarifu
kuwa Mungu aliweka vitu hivyo vinavyoitwa mianga ambavyo ndivyo utawala usiku
na mchana na kuweka mzunguko wa siku hivyo kuzaa mfumo wa majira na hatimaye
tunapata siku na miaka.Hivyo agizo la ibada linazingatia mapangilio huu wa
uumbaji na hivyo basi mwanadamu anaagizwa tumia siku ile ya mwisho ya
juma(Sabato)
Zaburi
19:1
Mbingu zahubiri utukufu wa Mungu,Na anga latangaza kazi ya
mikono yake. (Rumi 1:20)
Kutoka
20:8-11 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. (9)siku sita
fanyakazi, utende
mambo yako yote, (10) lakini siku ya Saba ni
Sabato ya BWANA,
Mungu wako, siku
hiyo usifanye kazi yeyote,wewe, wala mwana
wako, wala mjakazi
wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala
mgeni
aliyendani ya malango yako.(11)Maana, kwa siku sita
BWANA alifanya mbingu,
na nchi, na bahari, na vyote
vilivyomo,akastarehe
siku ya saba; kwahiyo BWANA akaibarikia
siku ya Sabato akaitakasa.
Baada ya kuona mchanganuo huo sasa tunaweza
kukubaliana na ukweli kuwa swala la ibada ni swala nyeti na rasmi sana na hivyo
lingepaswa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa kwasababu maandiko hayo ya Biblia
yanaonyesha wazi kuwa swala hilo la ibada ni swala la kimfumo, tena ni mfumo
ambao uliwekwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
JE’
SIKU HIYO YA IBADA (SABATO) NI IPI KATI YA SIKU HIZI ZA LEO?
Bilashaka hilo ndilo swali lililo kichwani mwako ndugu
msomaji wangu mpendwa!’,nami nimeona vema kupitia makala hii, niweke bayana
kila kipengele ili kufunua nuru hii ya wazi inayowekewa kisogo katika kipindi
hiki mfumuko wa imani na mifumo mbalimbali ya kidini.
Kanuni ya kiistoria na
maandiko ya kufahamu siku ya ibada.
Biblia inafunua
wazi siku hii ya kweli ya ibada katika maandiko ya kitabu cha Luka, na ili
kupata picha ya moja kwa moja juu ya swali hili kupitia andiko hilo la Luka’ ni
vyema kwanza tukumbushane historia:-
Jamii ya Wakristo wote tunaamini
kuwa Bwana Yesu alikufa na kufufuka, kumbukumbu ya kihistoria inayokubaliwa na
watu wote tangu karne na karne inaonyesha pasipo shaka kuwa Bwana Yesu aliuwawa
pale msalabani siku ya “Ijumaa’ na
kwa kuweka uzito wa ukweli wa hilo nikukumbushe pia kuwa katika siku hiyo
baadhi ya waumini wa madhehebu ya
Kikristo huadhimisha siku maalumu ianyoitwa Ijumaa kuu’ katika siku hiyo hawali
nyama kama ishara ya kuhuzunikia kifo hicho cha Yesu.’
Hivyo kwakuwa jamii
yote ya Waktristo inakubaliana kuwa Bwana Yesu alikufa siku ya ijumaa na
kufufuka siku ya jumapili, ndivyo pia inakuwa rahisi kuelewa juu ya siku hiyo
ya ibada inayotajwa na mandiko ni ipi katika mfululizo wa siku za juma kwa
kulinganisha na andiko hilo la Luka.
Luka
23:52 mtu huyu alikwenda kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu. (53)
akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi
lililochogwa mwambani, ambalo
hajalazwa mtu bado ndani yake.
(54)Na siku ile ilikuwa siku ya maandalio, na sabato ikaanza kuingia.
(55)Na wale wanawake
waliokuja naye toka Galilaya walikuwa
walimfuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili
wake ulivyowekwa. (56)
Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu.
Na siku ya
sabato
walistarehe kama ilivyoamriwa.
Andiko hilo la Luka
linataja kisa cha mauti ya Yesu na harakati za mazishi yake yaliyoendeshwa na Yusufu wa Al Mathaya, mtume Luka
anaripoti kuwa katika siku hiyo ambapo Bwana Yesu alikufa ( Ijumaa kuu), bwana mkubwa mmoja aitwaye Yusufu ndiye aliyeomba na kukabidhiwa
jukumu zima la mazishi ya Yesu katika siku
hiyo inayokubalika kihistoria kuwa ni siku ya Ijumaa.
Mtume
Luka anaitaja siku hiyo ya Ijumaa ya mauti ya Yesu kwa sifa ningine kuwa
ni siku ya maandalio, na ndipo hatimaye baada ya siku hiyo hufuatia siku ya
sabato’
Rejea:
Luka
23:...(54)Na
siku ile ilikuwa siku ya maandalio, na
sabato ikaanza kuingia.
Kumbuka
Bwana Yesu alikufa msalabani saa 9 jioni, muda ambao ulikaribiana na saa kumi
na mbili ambapo siku hubadilika, hata hivyo wakinamama wale walionekana wakijitokeza
katika kaburi hii inamaanisha kuwa muda ulikuwa umesogea zaidi, kwa kuwa
hatahivyo Biblia haitaji muda ambao Yusuph Al Mathaya aliondoka na mwili wa
Yesu kuelekea kaburini, kwahiyo ni wazi kuwa masaa hayo yalikaribia muda ambao
siku huisha na kuingia nyingine hasa kulingana na jukumu zito la kuushusha
mwili huo na kuanza safari ya kuupeleka katika kaburi lake’ naam siku ya sabato
ilianza kuingia.
Kwa uchambuzi huo
ndugu msomaji wangu ni bayana kuwa siku ya saba (sabato) inayokusudiwa ni
siku ya jumamosi ambayo kimsingi
ndiyo hufuatia baada ya siku ya Ijumaa.’
Maandiko ya Biblia
yanaweka wazi kuwa siku hiyo ya Sabato (Jumaamosi),
ndiyo iliyoamriwa kupumzika, na hivyo hata wale kina mama waliokuwa wafuasi wa
Yesu alirudi na kustarehe katika siku hiyo kama ilivyoamriwa.
Kidokezo:
Neno’
kama ilivyamriwa, lilimaanisha
kwa upande mwingine kuwa hakukua na amri nyingine iliyowahi kutolewa kubatilisha
hiyo ya kutunza sabato, na kwakuwa hiyo ya kutunza sabato bado ilitoka kwa Yesu
pia licha kwa muda huo alikwisha kufa, basi walilazimika kundelea na utii wao
kwa maelekezo hayo ya Yesu huku wakiwa wamezui shughuli ya kwenda kupaka
Marhamu mwili wa Yesu hadi itakapokwisha sabato.
Rejea:
Luka
23:…
(55)Na wale wanawake
waliokuja naye toka Galilaya
walikuwa
walimfuata, wakaliona kaburi, na jinsi
mwili wake ulivyowekwa. (56)
Wakarudi,
wakafanya tayari manukato na
marhamu. Na siku ya
sabato walistarehe kama
ilivyoamriwa
Katika sura ya 24’
ya Injili ya Luka, Biblia inaitaja siku ambayo Yesu alifufuka (jumapili) kama
siku ya kwanza ya juma’
Luka
24:1-2
Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza
kupambazuka,walikwenda
kaburini, wakayaleta
manukato waliyoweka tayari (2) Wakalikuta
lile jiwe limeviringishwa
mbali na kaburi.
Biblia inaitaja
siku hiyo ya jumapili kama siku ya kwanza ya juma, kwa maana hiyo siku ya saba ya juma ni Jumamosi, swali
la msingi linaweza kuibuka kuwa mbona basi majina ya siku hizi yanapingana na
mfumo wa asili! Kwa kuwa endapo tukihesabu siku kwa kufatisha utamshi mfumo
halisi wa siku hizo unabadilika, yaani kwa mfano:
tukitafsiri mosi (jumamosi) kuwa
ndiyo siku ya kwanza na pili (jumapili) ndiyo siku ya pili mfumo wa asili
unabadilika.
Lakini ni vyema
ieleweke kuwa majina hayo yaliyopachikwa siyo halisi na hayana uwiyano wowote
na hesabu ya kiasili ya siku, hata hivyo majina haya yalipachikwa tu karne
chache baadae na Wakoloni, na jambo la kushangaza ni kuwa mfumo huo tuliouzoea
wa uitaji wa majina ya siku kwa kusema Jumatatu, jumanne, jumatano alhamisi
ijumaa haukubalini hata na kalenda wala mfumo wa majina ya siku wa kiarabu.
Waarabu
wanavyotamka majina ya siku
1
|
Yaumu ahad
|
Sunday
|
Jumapili
|
2
|
Yaumu ithnain
|
Monday
|
Jumatatu
|
3
|
Yaumu thalathat
|
Tuesday
|
Jumanne
|
4
|
Yaumu al’baa’
|
Wenesday
|
Jumatano
|
5
|
Yaumu l khamsy
|
Thursday
|
Alhamisi
|
6
|
Yaumu
l-jamaa/ sittat
|
Friday
|
Ij umaa
|
7
|
Yaumu sabti
|
Saturday
|
Jumamosi/sabato
|
BWANA
YESU, MITUME NA WAKRISTO WOTE WA AWALI WALITUNZA SABATO (JUMAMOSI) KAMWE HAPAKUWA NA IBADA
NYINGINE.
Nijambo
linaloshangaza kwa mtu yeyote anayetangaza kuamini Biblia, kujikita katika
mfumo wa ibada nyingine yeyote tofauti na ile ya siku hii ya kweli ya saba ya
juma (sabato), hilo linatokana na kile kinachoonekana kuwa watu wote wa Biblia
manabii, mitume na waumini wote waliadhimisha mikutano yao mikuu ya ibada
katika siku hii ya saba ya juma Sabato (jumaamosi).
Hebu tupitie
ushahidi ufuatao kuthibitisha hili:-
YESU
ALITUNZA SABATO/JUMAAMOSI.
Luka
4:16
Akaenda Nazareti hapo alipo lelewa, na siku ya sabato akaingia
katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake.
Kwa andiko hilo
tunaona dhahili kuwa Bwana Yesu mwenyewe aliadhimisha matendo ya ibada katika
mfumo wake wa kawaida katika siku hiyo
ya saba ya juma, Sabato – Jumaamosi, na kimsingi Biblia haitaji siku nyingine
ambayo Yesu alitekeleza matendo ya ibada zaidi ya siku hiyo.
Kumbuka Yesu
alisema:
Mathayo
11:29
jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwakuwa mimi ni mpole na
mnyenyekevu wa moyo…
Hivyo ni vyema
kujiuliza kama ibada yako imejengwa katika imani na matendo yaliyoonekana kwa
mwasisi mwenyewe wa imani yaani Bwana Yesu Kristo!, na ikiwa sivyo ni vyema
kujichunguza upya na kufanya matengenezo.
Kwanini
Yesu mwenyewe alikuwa akisali siku hiyo?
Biblia inatoa
maelezo ya msingi yanayoonyesha sababu za msingi za Yesu mwenyewe kuhudhuria
ibada katika siku hiyo ya sabato.
Ebrania
12:2
Tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye
kutimiza iman Yetu.
Marko
2:28
Basi mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato pia
Hivyo kwa kifupi
alipaswa kunyesha kilelezo kama mwasisi
wa ibada ya kweli, na hivyo kuacha mfano
wa namna ibada ya kweli inavyopaswa kuwa.
MITUME
WALITUNZA SABATO/JUMAAMOSI.
Baada ya Yesu kupaa
mbinguni aliwaacha mitume wake ambao kimsingi ndiyo waliokuwa wakiendeleza
msingi wa imani aliyoicha Bwana na mwalimu wao Yesu Kristo, hivyo kadri ya
maandiko mitume hawa wanatajwa kuwa ni kioo cha msingi wa kweli wa imani. Bwana
Yesu alitamka maneno ya msingi sana yanayotia muhuri maelezo haya:-
Yohana awapokeaye
ninyi, anipokea mimi, naye anipokeaye mimi ampokea
yeye aliyenituma.
Kwakuwa mitume hao
walitarajiwa kufanya kile Yesu alichokianzisha, basi Bwana Yesu mwenyewe katika andiko hilo
anawatambulisha mitume hao kuwa wangestahili kupokelewa kwakuwa kuwapokea au
kuwaamini mitume hao kwa kile watakachofundisha na kutenda kadri ya mfano wa
Bwana na mwalimu Yesu Kristo il kuwa sawa na kusikiliza Bwana Yesu mwenyewe.
Ndipo kwa msingi
huu mtume Paulo aliwahi kutamka.
1Wakoritho
11:1
Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.
Tamko hili la mtume
Paulo linaonekana kugusa vizuri nyanja hii ya ibada kwa kile tunachosoma kadri
ya maandiko kuwa mtume huyo Paulo mwenyewe aliendeleza kanuni ileile ya ibada
ya Yesu kwa kuhudhuria ibada katika masinagogi na kuendesha mijadala ya kidini
siku ya Sabato.
Matendo
17:1
Waakisha kupita kati ya Ampifoli , na Apolonia
wakafika
Thesalonike, ambapo palikuwa na Sinagogi la
Wayahudi. (2) Na
Paulo, kama ilivyokuwa
desturi yake, akaingia mle walimo,
akahojiana nao kwa maneno
ya maandiko Sabato tatu.
Hivyo mtume Paulo
anasimama kama shuhuda wa kudumu kwa msingi wa ibada hiyo ya kweli ya siku ya
Sabato ya Bwana (Jumamosi), naye anafanya kilekile alichokifanya Yesu, yaani
kuhudhuria ibada za masinagogi kama ilivyokuwa desturi yake ndiyo uliokuwa
mfumo wake wa siku zote katika misha ya ibada.
Pamoja na ushahidi
huo wenye nguvu, bado Biblia inatoa ushahidi wa kutosha tu juu ya kudumu kwa
maadhimisho ya ibada kuu za mikusanyiko katika siku hii ya saba ya juma
(Sabato)katika vipindi mbalimbali vya mwendo wa safari ya imani wa mitume na
wajenzi wa kanisa la awali, tuone ushahidi wa maandiko mengine juu ya kudumu
kwa utunzaji wa siku hii ya kweli ya ibada Sabato katika ulimwengu wa kale wa
mitume na wafuasi wa Bwana Yesu mara baada ya kupaa kwake mbinguni.
Matendo
13:13-15..
lakini wao wakang’oa nanga wakasafiri
kutoka Pafo,
wakafika Perge
katika Pamfilia. Yohana akawaacha akarejea
Yerusalemu.
(14) Lakini wao wakatoka Perge, mji
mmoja wa
Pisidia, wakaingia katika Sinagogi
siku ya Sabato, wakaketi.
(15) Kisha, baada ya kusomwa Torati na chuo cha manabii
,
wakuu wa sinagogi
wakatuma mtu kwao, na kuwaambia,
Ndugu,kama mkiwa
na neno la kuwafaa watu hawa,lisemeni.
Hapa tena tunaona
mitume wakiadhimisha ibada katika siku hiyo ya Sabato, na kikubwa tunaona watu
waliokuwa katika Sinagogi walionyesha kutambua uwepo wao na kuwa karibisha
kutoa neno katika siku hiyo ya ibada ya Kibiblia, kwajumla mandiko ya Biblia
yako wazi sana katika hili nap engine niseme kuwa fundisho la siku ya ibada
ndilo fundisho la wazi sana na lenye ushahidi wa kutosha katika Bilblia, fanya
uamuzi wa kufata Biblia.
Ushahidi
mwingine / Kanisa lilitambua ibada ya siku ya Sabato pakee.
Uchambuzi wetu
utaishia katika kisa hiki cha safari ya watumishi wa Mungu wa awali katika
safari yao ya kuhimarisha makanisa, ambapo tunaona bado wakitoa picha ya kudumu
kwa maadhimisho ya ibada ya kweli katika siku hii ya Sabato:-
Matendo
16:4,5,13,16,17
Basi walikuwa wakipita katika
miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee waliyoko
Yerusalemu, ili wazishike. (5) Makanisa yakatiwa nguvu kwatika ile imani,
hesabu yao ikaongezeka kilasiku.
(13)Hata siku ya sabato
tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani yakuwa pana
mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
(16) Ikawa tulipokuwa tukienda
mahali pale pa kusali, kijakazi kimoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta,
aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. (17)akamfuata Paulo na sisi
akapiga kelele akisema, watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye
kuwahubiria njia ya wokovu.
Andiko hilo kwa
ujumla wake, lnaonesha hali halisi na picha ya mwenendo wa kanisa la mitume
namna lilivyodumu kutunza siku ya kweli ya ibada ya Sabato, Paulo na wenzake
wanaonekana kuchukua jukumu la kusafiri ili kuhubiri Injili na kuhimarisha
makanisa nyuma ya agizo la baraza la wazee na mitume lililoketi katika mji wa Yerusalemu
na kutoa maelekezo mbalimbali ambayo yangesaidia kuleta kuhimara na ukuaji wa
kanisa.
Katika ziara
inayoelezwa katika mafungu hayo, Paulo na wenzake wanaonekana kuendelea kudumu
kuadhimisha tendo la ibada katika siku hii ya kweli ya sabato, (Matendo 16:13)Hata siku ya sabato tukatoka
nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani yakuwa pana mahali pa
kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
Banafsi huwa
ninapatwa na uzuni kubwa sana ninaposoma maandika haya na kulinganisha na hali
tuliyonayo sasa ya mipasuko ya kidini iliyozaa siku mbalimbli za maadhimisho ya
ibada zisizo za kimaandiko.
Ni vyema ieleweke
kuwa kama Yesu angefanya au kuamuru mabadiliko yeyote juu ua siku ya ibada,
basi watu wa kwanza ambao wangetekeleza ni mitume wake ambao kimsingi waliishi
muda kadhaa mara baada ya kifo na ufufuko wa Yesu.
TUNAWEZAJE
KUJUA KUWA SABATO HII’ JUMAMOSI NDIYO HALISI?
Mhubiri
3:11 kilakitu amekifanya kizuri kwa
wakati wake’ tena ameiweka hiyo
milele ndani ya miyoyo
yao; ila kwajinsi mwanadamu asivyoweza
kuivumbua kazi ya Mungu
anayoifanya tangu mwanzo hata
mwisho.
14 Najua
yakwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele,
haiwezekazi kuzidisha kitu, wala kuipunguza
kitu, nayo Mungu
ameifanya ili watu wamche
kitabu hicho cha
mhubiri kinatoa majibu ya swali hilo muhimu kwa kuonyesha njia na kusudi la
Mungu mwenyewe kulinda yale aliyoyaweka yeye mwenyewe ili yasiharibiwe na
yeyote.
Andiko hilo
linaonyesha kuwa Mungu hutumia miyoyo ya wanadamu wenyewe kuhifadhi maarifa ya
uzuri wa kazi yake, na kwa kadri ya historia tunaweza kuona jinsi mwanadamu
mwenyewe alivyoshiriki kulinda mifumo muhimu ya uumbaji wa Mungu hususani
mzunguko wa siku:-
Historia
inaonyesha:
Tangu karne nyingi watu walitunza
mzunguko wa siku bila kupoteza mwelekeo kwa kutumia SOLAR CALENDER – yaani
kalenda ya asili ya mfumo wa mzunguko wa dunia wa uumbaji, unaohusisha Jua,
Planets, and other bodies – na viumbwa anga vingine vinavyofanya mzunguko wa
dunia.
Kwajumla katika katika mfumo huu
wa asili mwenendo wa jua ndiyo uliotoa mwelekeo wa hesabu ya mzunguko wa masaa,
hivyo kupata siku miaka na miezi.
§ Mwaka 350
kk, ilitumika njia ya asili ya kufata kivuli cha binadamu kinavyosogea kwa
kufuata mwanga wajua.(watu walitunza mzunguko wa masaa na siku kwa njia hiyo).
§ Karne ya
4’ mjapani Lntern Clock aligundua saa ya kutumia mashine iliyoitwa Horogum
kabla ya kuitwa Clock
§ Ndipo
karne ya 8’ saa kongwe ilibuniwa na kuanza kutumiwa ambayo imehifadhiwa katika
jumba kongwe kule Misri.
§ Na baadae ilifatia saa nyingine ya mjapani
Enly De Vick, ambayo ilitumika katika jengo la mahakama kule Ufaransa ikiwa na
Urefu wa futi 37’ na kilo 237’
§ Wataalamu
wengine waliongezeka kama vile: mzungu George Graham, Mholanzi Christian Hygens
na baadae kugundulika teknolojia ya kutengeneza mizani na mwanafizikia Robelt
Hook.
Kutokana na
teknolijia ile ya asili na ile ya saa kusaidia kutunza hali ya mzunguko wa siku
ndiyo maana historia pia imefanikiwa kutunza kumbukumbu ya tarehe ama miaka ya
matukio muhimu duniani.
Wanahistoria
wanagawa miaka katika makundi mbalimbali ikiwa ni matokeo ya uwezekano wa kunza
rekodi ya mzunguko wa dunia;-
Mgawanyo
wa siku na miaka kihistoria:-
Day – duration
of twenty four hours / Kipindi cha masaa ishirini na nne.
Week
– duration of seven days/ kipindi
cha siku saba
Year
– duration of twelve months/
kipindi cha miezi kumi na mbili.
Decade
– duration
of ten years/kipindi cha miaka kumi.
Century
– duration of one hundred years/kipindi
cha miaka miamoja.
Millennium
– duration
of one thousand years/ kipindi cha miaka elfu moja.
Age –
a period
based on man’s economic activities and the types of tools
Kwa mtu mwenye
kutafakari atakubaliana na ukweli kuwa tendo la kuwezekana kutunzwa na
kumbukumbu za matukio sahihii kwa miaka na karne nyingi za nyuma ni ushahidi
tosha kuwa hakuna makosa yeyote juu ya maadhimisho yanayofanywa na waumini wa
dunia nzima ya kuadhimisha mikutaniko ya ibada katika siku hii ya kweli ya
sabato kadri ya mfumo wao wa kijografia wa mzunguko wa siku.
No comments:
Post a Comment