Wednesday, December 12, 2012

Nabii Daniel alionyeshwa njozi ya mambo ambayo yangetokea katika kipindi cha historia ya ulimwengu huu, katika njozi iliyositaajabisha sana. Wanyama waliibuka toka baharini, wakiashiria falme zenye uwezo na mamlaka ya kiulimwengu, zenye kutawala
mamlaka za mataifa mengine ulimwenguni. Wanyama hawa waliibuka kwa awamu, ikiashiria mfuatano wa mamlaka hizi zenye nguvu za kiulimwengu katika kutawala mataifa mengine.

Daniel 7:4
Kwanza kabisa, Daniel aliona upepo ukivuma katika bahari, na Simba mwenye mabawa mawili ya tai mkubwa yaliyofutuka akaibuka toka baharini. Daniel 7:4 ~ ikiashiria ufalme wa Babel
Daniel 7:5 
Pili Upepo ulipovuma, Daniel akaona mnyama mfano wa Dubu na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake


No comments:

Post a Comment